Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), ameihakikishia jumuiya ya wafanya biashara na wajasiriamali nchini kwamba Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kukuza biashara zao.
Mhe. Luswetula ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na jumuiya ya wafanyabiashara mjini Mpanda mkoani Katavi ambapo amesisitiza kuwa hatua hiyo imelenga kuongeza tija katika biashara na mapato ya Serikali kwa ujumla Kupitia ulipaji kodi.
Alisema kuwa Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefanya kazi kubwa ya kusisimua biashara na kuagiza ulipaji kodi usio wa tumia nguvu hatua iliyosababisha mapato yatokanayo na kodi kuongezeka kwa kiwango kikubwa.
“Tumemsikia Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Yusuph Mwenda akiutangazia umma kuhusu mafanikio waliyoyapata ya kukusanya kodi ambapo kwa mwezi Desemba peke yake. TRA imekusanya zaidi ya shilingi trilioni 4.13, rekodi ambayo hajawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru” alisema Mhe. Luswetula
Aidha, aliwataka wafanyabishara kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi kwa kulipa kodi kwa hiari, kwani fedha hizo hutumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ikiwemo barabara, elimu, afya, maji, nishati, miundombinu ya reli na miradi mingine.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa mkoa wa Katavi, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Bw. Amani Mahela, iliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na ulipaji kodi na kushauri hatua zaidi ziendelee kuchukuliwa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi ikiwemo kusamehe madai ya kodi ya miaka mitano iliyopita.
Alisema kuwa ulipaji wa kodi kwa hiari unatokana na wadau kuona matunda ya kodi husika kutumika katika ujenzi wa miradi ya kimkakati ya kuboresha huduma za jamii na kiuchumi na kusisitiza kuwa ili kufanikisha zaidi matokeo ya ulipaji kodi ni muhimu Serikali iongeze idadi ama wigo wa walipa kodi ili angalau ilingane na idadi ya watu milioni 62 waliopo hivi sasa.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akizungumza jambo wakati alipofanya Mkutano na Jumuiya ya Wafanyabiashara na wajasiriamali mjini Mpanda Mkoani Katavi, ambapo aliwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kukuza biashara zao.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Mkoa wa Katavi, Bw. Nicholaus Migera akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ya kikodi wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali mjini Mpanda Mkoani Katavi, ambapo Mhe. Luswetula aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kukuza biashara zao.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wakifualitia hotuba ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (hayupo pichani), wakati alipokutana na kufanya Mkutano na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali mjini Mpanda Mkoani Katavi, ambapo Mhe. Luswetula aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kukuza biashara zao.
Baadhi ya Wafanyabiashara wakitoa maoni wakati wa Mkutano na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (hayupo pichani), na Jumuiya ya Wafanyabiashara mjini Mpanda Mkoani Katavi, ambapo Mhe. Luswetula aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kukuza biashara zao.






