MEYA DKT.NICAS ATOA SIKU SABA KUTOKOMEZA KERO YA NZI VISIGA

Na Khadija Kalili, Kibaha
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas Mawazo ametoa siku saba kwa Shamba la Kuku la lililopo Mtaa wa Madafu Kata ya Visiga Wilayani Kibaha kupulizia dawa ya kuua nzi ambao wamekuwa kero kwa wananchi katika Kata hiyo.
Mstahiki Meya Dkt. Nicas amsimamo huo baada ya wananchi kulalamikia shamba hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Visiga Kati wakati akiwa kwenye ziara ya kutatua kero za wananchi kwenye Kata ya Visiga.
Sabra Selemani ambaye ni mwanach amelalamika kuwa shamba hilo linalazisha Nzi kutokana na uchafu wa kinyesi cha kuku (mbolea) ambayo imekuwa ikikaa muda mrefu huoza na kuanza kutoa harufu mbaya.
Sabra amesema kuwa mbolea hiyo ikioza inazalisha funza ambao huzaa Nzi kwa wingi ambao husambaa kwenye baadhi ya Mitaa na kusababisha kero kubwa kwa wananchi hasa waleRC wanaofanya biashara za vyakula na wakati mwingine huingia kwenye vyakula vyao hali inayowakimbiza wateja wao.