DKT. MWIGULU AFUNGUA SKULI YA CHUKWANI, ZANZIBAR

_Ampongeza Dkt. Mwinyi kwa uwekezaji katika sekta ya Elimu._

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 05, 2026 amefungua Skuli ya Sekondari Chukwani, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Ujenzi wa skuli hiyo ambayo imegharimu shilingi bilioni 6.1 imeanzishwa kwa lengo la kuwaandaa vijana wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na

maadili, kwa kuunganisha nadharia na vitendo na hivyo kuwa na manufaa mengi ikiwemo kuongeza fursa za elimu bora kwa watoto wa Zanzibar.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya elimu.