MRADI UKUZAJI SAMAKI CHATO KUINUSURU HIFADHI YA KISIWA RUBONDO

……….

CHATO

UKAMILISHWAJI wa kituo cha utafiti na ushauri wa ukuzaji wa viumbe maji wilayani Chato mkoani Geita, umetajwa kuwa suluhisho la uharifu wa mazao ya samaki ikiwemo uvamizi wa hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo.

Hatua hiyo inatazamiwa kwenda Sambamba na uanzishwaji wa uvuvi wa vizimba kwa lengo la kuongeza uzalishaji, uhifadhi wa mazingira na uongezaji tija wa pato la mtu, kaya na taifa kwa ujumla.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally, amesema kukamilika kwa mradi mkubwa wa kuendeleza ukuzaji wa viumbe maji Rubambangwe utakuwa msaada mkubwa kwa wavuvi waliopo ukanda wa ziwa Viktoria.

Nikutokana na mradi huo kuzalisha vifaranga vya kutosha na vyenye ubora unaostahili kuwahudumia watanzania kupata chakula na kuongeza kipato.

Hata hivyo Dkt. Bashiru amedai kuwa uanzishwaji wa uvuvi wa vizimba utakuwa suluhisho kwa uvamizi wa maeneo ya hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo.

Awali msimamizi wa mradi huo, Elinsa Massawe, amesema mradi huo ulianza kujengwa tangu mwaka 2020 na kwamba umefikia aslimia 75 na unatazamiwa kuwa na mabwawa makubwa 9 kwaajili ya kutotoreshea vifaranga vya samaki.

Sambamba na hilo, kitakuwa kituo cha kutoa elimu na mafunzo mafupi kwa wavuvi na wanafunzi wanaosomea taaluma ya uvuvi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Aidha mpaka sasa tayali vifaranga 1,500 vimepandikizwa ili kupata samaki wazazi watakaochujwa na kutengwa eneo maalumu kwaajili ya kupata mbegu bora zitakazosaidia kuzalisha samaki wakubwa kabla ya kupelekwa kwa jamii.

                          Mwisho.