Video: Kikwete Asema Urais ni Mpango wa Mungu, Afafanua Nafasi ya Kiongozi




Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, amesema suala la kuwa kiongozi hususan urais ni mipango ya Mungu.

Kikwete amesema tume iliyoundwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume mwaka 2001 ambayo alikuwepo yeye, Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa), Dkt. Ali Shein na Marehemu Adam Mwakanjuki.

Ametoa kauli hiyo wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Uhamiaji na Makazi ya Askari lililopo wilayani Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni sehemu ya sherehe za Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.