Raia wa China waliodakwa Osterbay na mamilioni wafikishwa mahakamani

Dar es Salaam. Raia wawili wa China, Weisi Wang (44) na Yao Licong (32), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka mawili, ya kuongoza genge la uhalifu na kutakatisha fedha zenye thamani ya Dola 707,075 za Marekani pamoja na fedha za Kitanzania Sh281 milioni.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo, Jumatano, Januari 7, 2026, na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi, huku jopo la mawakili watatu likiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, akishirikiana na Roida Mwakamele na Benjamini Muloto.

Mashtaka hayo yamesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki. Kesi imeahirishwa hadi Januari 21, 2026, na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Washtakiwa hao walionekana katika video iliyosambaa mtandaoni jana, wakiwa ndani ya geti baada ya kukamatwa, huku wakitoa hela kwenye mifuko (shangazi kaja).

Endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi.