TAKUKURU YAKAMATA RAIA WA CHINA WAKIWA NA FEDHA HARAMU

………

Taasisi ya Kuzuia Na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Dar es salaam imewakamata Raia wa China Yao Licong na Wang Weisi wakazi wa Oysterbay Apartments Kinondoni Dar es salaam wakiwa na fedha haramu zaidi ya shilingi bilioni mbili.

 

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee amesema kuwa ukamataji huo ni hatua ya matokeo ya oparesheni maalumu ya uchunguzi dhidi ya uhalifu unaohusisha matumizi ya taarifa za kadi za benki zilizoibiwa kujipatia fedha haramu.

 

Nyakizee amesema mpaka sasa watuhumiwa zaidi ya 137 wamekamatwa, kupekuliwa na kuhojiwa katika  mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro,Dar es salaam, Mwanza na Visiwa vya Zanzibar 

Aidha Mkuu huyo wa TAKUKURU Kinondoni  amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa zaidi ya shilingi bilioni 18 zimetakatishwa kwa utaratibu huo  Kwa kipindi Cha miaka minne kuanzia mwaka  2022 Hadi 2025

 

TAKUKURU tashadhari kwa baadhi ya Watanzania wenye tamaa ya kutaka kutajirika Kwa haraka kwa njia zisizo sahihi,kuacha mara Moja kusajili makampuni hewa wao wenyewe au Kwa kushirikiana na raia wa kigeni Kwa lengo la kutumia taarifa za kadi zilizoibiwa ili kujiingizia kipato haramu.