MAKAMU WA PILI WA RAIS KUZINDUA MASHINDANO MAKUBWA YA QUR’AAN DUNIANI

::::::::

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano makubwa zaidi ya Qur’aan Tukufu duniani yanayoandaliwa na Taasisi ya Alhikma Foundation.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwaka 2026 kwa mara ya 26 tangu kuanzishwa kwake, yakihusisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Akizungumza Leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Alhikma Foundation, Sheikh Nurdeen Kishki, alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika kwa asilimia 90.

Alisema taasisi hiyo inaendelea na utekelezaji wa mipango kwa kuzingatia ratiba, huku akisisitiza kuwa hakuna ucheleweshaji wowote.

Mashindano hayo yatazinduliwa rasmi Februari 1, 2026, na mgeni maalumu atakuwa Sheikh Abdul Rashid Ali Sufi kutoka Qatar, huku taarifa kamili za mashindano zikitangazwa baada ya uzinduzi.