……………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Dkt Moses Kusiluka imewataja viongozi walioteuliwa kuwa ni pamoja na Paul Christian Makonda kuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na michezo,ambapo kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo.
Aidha amemteua Profesa Palamagamba John Aidan Kabudi kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum) ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na michezo.

