SHAURIMOYO NA LINDI HALI SHWARI, USAFI WA MAZINGIRA WABORESHA.

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam DAWASA wamekamilisha kazi ya usafishaji miundombinu ya majitaka mtaa wa Shaurimoyo na Lindi Kata ya Kariakoo.

Kukamilika kwa kazi hiyo kutaboresha Mazingira ya utendaji kazi kwa wafanyabiashara wa spea za magari katika mtaa huo kumaliza harufu iliyosababishwa na utiririkaji wa majitaka kiholela.

Mamlaka inasisitiza matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka kwa kutotupa taka ngumu katika mifumo hiyo na kuwaasa wananchi kutoa taarifa za mara kwa mara pindi inapotokea changamoto ya utiririshaji majitaka.