HATIMAYE mechi ya malkia wawili, JKT Queens na Simba Queens imemalizika kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya raundi ya saba inakumbushia mechi ya Desemba 10 mwaka jana matokeo yakiisha kwa sare hiyo hiyo mechi ikipigwa Uwanja wa KMC Complex Mwenge.
JKT ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa winga machachari, Winifrida Gerald baada ya kupokea pasi kutoka kwa mshambuliaji Stumai Abdallah.
Simba ilichomoa bao hilo dakika ya 53 kupitia mshambuliaji, Zawadi Usanase aliyepiga friikiki.
Sare hiyo inaifanya Simba iendelee kusalia kileleni na pointi 19, ikifuatiwa na Yanga Princess yenye pointi 18 na JKT ikiwa ya tatu na pointi 17.
Hii inakuwa sare ya kwanza kwa Simba msimu huu katika mechi saba, imeshinda sita kwa upande wa JKT inakuwa sare ya pili ya kwanza ya kwanza 1-1 na Fountain Gate Princess ikishinda mechi tano.
