TCAA Yaendelea Kutoa Elimu ya Usafiri wa Anga Kupitia Maonesho ya ZITF Zanzibar

 

Afisa Muongozaji Ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Fadhil Nkomally akielezea jinsi huduma za Uongozaji Ndege zinavyofanyika kwa Mwananchi aliyefika katika Banda la TCAA katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar, yanayoendelea kufanyika katika Kituo cha Maonesho kilichopo Dimani, Zanzibar.
Mgeni akisaini kitabu cha katika Banda la TCAA katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar, yanayoendelea kufanyika katika Kituo cha Maonesho kilichopo Dimani, Zanzibar.
Mkaguzi wa Ndege Nyuki (Droni) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Alex Kadiva akitoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi salama na yenye kuzingatia sheria za Ndege Nyuki (Droni) katika Banda la TCAA katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar, yanayoendelea kufanyika katika Kituo cha Maonesho kilichopo Dimani, Zanzibar.