Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Khamis Said akifafanua jambo katika kikao kazi maalum cha kujadili utekelezaji wa miradi yaelimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
*************
Zanzibar
Katika kuendeleza ushirikiano na wadau wa Sekta ya Elimu nchini, Mamlaka ya ElimuTanzania (TEA) kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF Tanzania) wamefungua rasmi milango ya utekelezaji wa miradi ya elimu visiwani Zanzibar kupitiaWizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA), kwa lengo la kuboresha miundombinuya elimu.
Kupitia ushirikiano huo, TEA na UNICEF wametenga jumla ya shilingi bilioni 2.5 kwa ajiliya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara za sayansi pamoja namatundu ya vyoo katika shule 20 ambapo, shule 11 zipo kisiwani Unguja na shule 9 kisiwani Pemba.
Akizungumza wakati wa kikao kazi maalum cha kujadili utekelezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha alisema, utekelezaji wa mradi unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari nakukamilika kabla ya mwezi wa sita mwaka huu.
Dkt. Kipesha alibainisha kuwa lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanafunzi kusomakatika mazingira bora, salama na rafiki kwa afya zao. Aliongeza kuwa TEA ni taasisi yaMuungano hivyo utekelezaji wa miradi ya elimu Zanzibar ni sehemu ya majukumu yakeya msingi.
Aidha, alisisitiza kuwa ushirikiano uliopo kati ya TEA na Wizara ya Elimu na Mafunzo yaAmali Zanzibar umekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya miradi mbalimbali ya elimuinayotekelezwa na ambayo imekamilika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Said, aliishukuru TEA kwa mchango mkubwa kwenye uboreshaji wamiundombinu ya elimu huku akieleza kuwa miradi hiyo imekuwa kichocheo cha wadauwengine kujitokeza kusaidia maendeleo kwenye sekta ya elimu.
Bw. Said aliongeza kuwa ukarabati na ujenzi wa miundombinu hiyo umefika wakatimuafaka kwani majengo mengi ya shule hizo ni ya kizamani na yako katika haliisiyoridhisha. Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutachangia kuinua kiwango cha taaluma kwani wanafunzi watapata motisha ya kusoma katika mazingira ya kisasa.
“Wizara inatoa shukrani za dhati kwa TEA kwa ushirikiano mkubwa mnaoendeleakutupatia katika kuboresha miundombinu ya elimu na tunawaahidi kusimamiautekelezaji wa miradi yote kwa ufanisi ili ilete tija kwa maendeleo ya sekta ya elimu,” alisema Bw. Said.
Kwa sasa TEA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya miundombinu ya elimuZanzibar kama taasisi ya Muungano. Awali, jumla ya shilingi bilioni 3.2 zilitengwa kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya mafunzo ya amali ambayo utekelezaji wake badounaendelea huku shilingi bilioni 2.5 zikitengwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wamadarasa, maabara za sayansi na matundu ya vyoo.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania Dkt. Erasmus Kipesha akitoamaelezo kuhusu ufadhili wa miradi ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu kwashule za Unguja na Pemba visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA Bw. Masozi Nyirenda akisistiza jambo kuhusu utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwana TEA kwa upande wa Zanzibar.
Baadhi ya wataalamu kutoka TEA na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakifuatilia majadiliano kuhusu utekelezaji wa miradi ya uboreshajimiundombinu kwenye shule za Unguja na Pemba unaotarajia kuanza Januari mwishoni 2026.
Muonekano wa maabara ya sayansi itayofanyiwa ukarabati katika shule yaSekondari Chwaka iliyopo Wilaya ya Kati, Kusini Unguja
Muonekano wa vyumba vya madarasa vitakavyofanyiwa ukarabati katika shule yaSekondari CharaweWilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
Muonekano wa matundu ya vyoo yakayojengwa upya shule ya Sekondari Kijini iliyopo Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja



