Amebainisha hayo Januari 9, 2026 Jijini Arusha, wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Menejimenti ya Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, ambapo Mhe. Kapinga amesema maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha taasisi zote zinafanyiwa tathmini za mara kwa mara ili kubaini changamoto, kuboresha mifumo ya utendaji na kuongeza uwajibikaji.
Aidha, Amesema Mpango wa utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 unaonesha kuwa asilimia 22 ya fedha za utekelezaji zitatoka Serikalini, asilimia 8 kutoka Mashirika ya Umma, huku asilimia 70 ikitarajiwa kutoka sekta binafsi, hali inayozitaka Taasisi zenye viashiria vya kujitegemea kupunguza utegemezi kwa Serikali na kuongeza ubunifu pamoja na ufanisi.
Vilevile, amezielekeza Taasisi zote chini ya Wizara hiyo kuhakikisha ndani ya siku 100 zinakuwa na mifumo rafiki ya kupokea, kushughulikia na kutoa mrejesho wa changamoto kutoka kwa wananchi na wadau, hatua itakayoongeza uwazi na imani kwa taasisi za umma.
Katika kuongeza ajira na tija, Waziri Kapinga amesema Wizara itaendelea kutegemea Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) katika matumizi ya teknolojia zinazohusiana na mazao ya kimkakati kwa kuzingatia mkoa husika, hatua itakayochochea ajira kwa vijana wengi, na kwa Wakala wa Vipimo (WMA) amewataka kushuka chini kuwasaidia wananchi kuongeza thamani na vipato vyao, akisisitiza kuwa jukumu hilo lisiachwe kufanywa na taasisi nyingine
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Abdallah amesema kikao hicho ni muhimu kwa viongozi kwani kinawajengea uwezo kuhusu maadili ya utumishi wa umma, nidhamu, uongozi na afya ya akili, ikiwa ni sehemu ya maono ya Waziri katika kuimarisha utendaji kazi wenye tija ndani ya Wizara.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
