KUTOKANA na majeraha aliyopata Aziz Andabwile ambaye Kocha Pedro Goncalves alikuwa akimtumia eneo la beki wa kati, sasa jukumu hilo amempa Moussa Bala Conte.
Conte ambaye naye ni kiungo mkabaji kama ilivyo kwa Andabwile, katika mechi mbili zilizopita za Kombe la Mapinduzi 2026 dhidi ya TRA United na Singida Black Stars, alicheza beki wa kati sambamba na Frank Assinki.
Dhidi ya TRA United ambayo ilikuwa mechi ya kwanza kwa Conte kucheza, alitokea benchi akiingia dakika ya 63 kuchukua nafasi ya Nizar Abubakar Othman ‘Ninju’, kisha dhidi ya Singida Black Stars akicheza dakika zote tisini.
Wakati Conte akicheza beki wa kati, eneo la kiungo mkabaji yupo Mohamed Damaro anayecheza pacha na Duke Abuya aliyepewa kitambaa cha unahodha katika michuano hii.
“Amefanya vizuri kwani mechi zote hizo amechangia timu kutoruhusu bao, hivyo utaona ni kwa namna gani ameifanya kazi kwa ufasaha,” amesema Pedro.
