CCM KUFANYA MAPITIO SHERIA IDADI NYUMBA ZINAZOPASWA KUSIMAMIWA NA MABALOZI


-Lengo ni kuwapunguzia mzigo wakati wa kutekeleza majukumu yao

Na Said Nwishehe,Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiro ameeleza kuwa Chama hicho kitafanya mapitio ya sheria kuhusu idadi ya nyumba zinazopaswa kusimamiwa mabalozi Ili kuwapunguzia mzigo wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Dk.Migiro ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa mashina wa Wilaya za Kinondoni na Ubungo mkoani Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mkoa huo yenye kauli mbiu inayosema Shina lako linakuita.

Akifafanua kuhusu hatua hiyo ya kufanya mapitio ya sheria ni kwamba inalenga kuwaondolea mzigo wa usimamizi viongozi hao ili kuwawezesha kubaini na kudhibiti uhalifu pamoja na kufuatilia wageni wanaoingia katika maeneo yao.

“Kufanya tathmini ya ukubwa wa shina kutaongeza weledi katika kuwahudumia wananchi pamoja na kusimamia vema shughuli za maendeleo ya wananchi,”ameeleza Dk.Migiro mbele ya mamia ya viongozi hao.

Amesisiza shina ni mtima wa CCM na ndipo mambo yote yanapoanzia na kuishia.”Tutafanya tathmini ya ukubwa wa mashina ili kumuwezesha balozi kufanya majukumu yake ipasavyo.


Ameyataja baadhi ya majukumu hayo ni kukusanya maoni ya wanachama pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama.

Wakati huo huo Dk.Migiro amewataka viongozi kuwa mfano bora wa kushiriki kwenye ngazi hizo.Ndugy zangu mabalozi CCM ni Chama kikubwa kwasababu ya watu wake na leo tumeona watu hawa na naamini wapo wana CCM,wapenzi wa CCM na wananchi wenzetu wengine.”

“Tujue tunapoimarisha Chama chetu cha Mapinduzi tunaimairisha ustawi wa Taifa letu kwahyo tunakila sababu ya kushirikiana kama makundi mbalimbali kuleta mshikamano wa kitaifa.”

Aidha amesema umoja wetu kama Taifa ndio ushindi kwa vizazi vya sasa na vijavyo hivyo wanapofanya kazi za Chama utu, heshima na maadili ni muhinu kupewa kipaumbele kwasababu hivyo ndivyo vifakifanya Chama cha Mapinduzi kuendelea kuaminiwa,kutegemewa na kuthaminiwa.