MWANAMKE MMOJA AFARIKI DUNIA AJALI YA ROLI MBEZI KWA MSUGULI

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya gari aina ya roli lenye namba ya usajili T696 CLY kuacha njia na kumgonga mwanamke huyo katika maeneo ya mataa ya Mbezi kwa Msuguli Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashahidi gari hilo liliacha njia likijarabu kuwakwepa madereva pikipiki ambao walikuwa maeneo hayo na kusababisha kumgonga mtu huyo na kufariki hapo hapo.