Akizungumza leo Januari 10,2025 Ikulu Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo mbalimbali na hasa Wachezaji wa Taifa ya Taifa ,Rais Samia amesema anawapongeza kwa dhati kabisa Taifa Stars kwa kufuzu na kufika hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2025.
“Mafanikio haya ni makubwa na niushahidi soka letu sasa linaendelea kupanda barani Afrika kwa mara ya kwanza nilikaa kwenye televisheni mwanzo mwisho .Siku hiyo nilikuwa nimefunga nikaa kufutari wakati naendelea na futari zangu mchezo (Tanzania na Moroco)unataka kuanza nikaa nikaangalia watoto wangu kazi wanayofanya
“Lakini nimekaa pale nimeangalia mwili wote unauma maana wakipigwa au wakizuiwa mimi eeeehee …wakiwekewa miguu wakisumwa mimi eeee mbona wataniumizia wanangu ,nimeondoka pale mwili unaniuma lakini hongereni mmefanya kazi nzuri sana.
“Na tunajua kwanini yale yalitokea ni kwasababu tunajua tuliocheza nao ni wenyeji, ni taifa lenye fedha , ni taifa ambalo linaushawishi kwa wenzetu hao kwasababu tulikuwa tunaona wazi na Dunia imeona wazi Tanzania ni wapambanaji .Wamepambana lakini lile lililotokea ilikuwa lazıma itokee iwe iwavyo
“Kwahiyo hawawapongeza mmefanya vizuri sana .Nawapongeza pia benchi la ufundi, viongozi wa timu.Ni ukweli michezo yetu imepanda lakini michezo mingine pia imepanda inakwenda juu.
Wakati huo huo Rais Dk.Samia amewapongeza wanamichezo wa timu za Taifa ambapo ameipongeza pia Aidha nizipongeze timu za Taifa niipongeze timu ya Taifa ya Kriketi kwa kushiriki Kombe la Dunia.
“Lakini niipongeze timu ya mpira wa miguu ya watoto wangu wanawake kwa kushiriki Kombe la Dunia nchini Ufilipini hongereni sana.Pongezi pia ziende kwa mabondia wetu waliotwaa makombe ikiwemo timu ya Taifa ya ridhaa iliyopata medali 18 ikiwemo moja ya dhahabu medali za fedha nne na 13 za shaba katika mashindano ya kanda ya tatu ya Afrika yaliyofanyika Nairobi Kenya
“Tunakwenda ndugu zangu tulikotoka sio tuliko leo angalau jina la Tanzania linasikika ,linaonekana kila kwenye fani.Pia niwapongeze kwa ushiriki wa Kombe la Dunia lililofanyika Dubai ambako bondia wetu mmoja alifika hatua ya 16 bora.”
Pia Rais Samia ametoa pongezi kwa timu za Taifa zilizofanya vizuri ukanda wa CECAFA kwa upande wa timu za shule , timu za kuogelea na timu za watu wenye ulemavu zote anazipongeza wamebeba bendera za nchi ya Tanzania.
Ameongeza kwa upande wa ridhaa amempongeza mwanariadhaa Alphonce Simbu kwa kushinda medali ya dhahabu ya Tokhyo marathon 2025 akiwa Mtanzania wa kwanza kutwaa medali ya dhahabu.
“Lakini pamoja naye nimpongeze kijana wetu Cecilia Panga kutwaa dhahabu ya mbio za kilometa 15 zilizofanyika Sao Paulo nchini Brazili kwa kutumia muda wa dakika 51.8 .Hawa ni Watanzania waliopeperusha bendera yetu kwenye riadhaa .
“Nilikuwa namuangalia Simbu akipongezwa anasema amejaribu mara kadhaa lakini safari hii lazıma mimi na medali mara hii lakini akawa na manung’uniko anasema ni jitihada zangu binafsi serikali inamkono kidogo lakini sana binafsi , nikuhakikishie tumeona tutakusapoti huko mbele.
Pamoja na hayo Rais Dk.Samia amesema nidhamu walionesha wanamichezo wote ni alama ya uzalendo na wameipeperusha vema bendera yetu na wameandika historia mpya katika taifa letu na katika ulimwengu wa michezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanaume ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Rais Mhe. Dkt. Samia aliwaandalia hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza Wanamichezo waliofanya vizuri Kimataifa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2026. Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ilishiriki kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ nchini Morocco na kufika hatua ya mtoano ambayo ni historia kubwa kwa Tanzania tangu ilipoanza kushiriki michunohiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanamichezo mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza mara baada ya kufanya vizuri katika Mashindano ya Kimataifa, tarehe 10 Januari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanaume ‘Taifa Strs’ iliyosainiwa na Wachezaji kutoka kwa Nahodha msaidizi wa Timu hiyo, Bakari Nondo Mamnyeto kwenye hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2026.