Naibu waziri wa maji Eng.Kundo Mathew amemuelekeza katibu mkuu wizara ya maji Kumfatilia mkandarasi aliyekabidhiwa mradi wa kuondosha maji taka uliopo katika kata ya Katende halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita na kuhakikisha anaondolewa kabisa katika mikataba ya wizara hiyo.
Ni wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa kuondosha maji taka na kukuta umetelekezwa na mkandarasi huyo ambaye hakuepo eneo la kazi.
Mradi wa kuondosha maji taka katika wilaya ya chato unaghalimu kiasi cha takribani shilingi bilioni 1.5 ambapo mpaka sasa mkandarasi ameshakabidhiwa takribani shilingi milioni 800 na kuutelekeza mradi huo.
Wilaya ya chato ina uhitaji mkubwa na mradi huo hususani kipindi cha mvua kutokana na kusambaa kwa maji taka katika maeneo mengi hivyo kuwaibua viongozi katika wilaya hiyo kumuangukia naibu waziri juu ya kukamilika kwa mradi huo.
Diwani wa kata ya Bungila Batromeo Christian amesema kuwa mradi huo ulinzishwa mnamo mwaka 2022 lakini mpaka sasa bado unasuasua huku mkandarasi akiwa ameshakula fedha nyingi.

.jpeg)

