Takribani wanafunzi 600 katika kata ya Kalangalala wenye Hali ya chini wanakadiliwa kupata madaftari kwa ajili ya kuanza nayo msimu mpya wa masomo 2026.
Kata ya kalangalala Ina jumla ya shule za msingi 9 na shule za sekondari mbili ambapo jumla ya wanafunzi 1640 katika kata hiyo wameandikishwa kuanza darasa la kwanza.
Muitikio huo wa uandikiashwaji umemuibua diwani wa kata ya Kalangalala Ruben Sagayika kugawa madaftari pamoja na kalamu kwa Wanafunzi wanaotarajiwa kufungua shule Januari 13.
Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo amesema zoezi la ugawaji wa madaftari litakuwa endelevu katika kata hiyo ili kuhakikisha Kila mtoto anafika shuleni akiwa na vifaa vya shule.
“Tutakuwa pia tunapitia kwenye mashule tunaangalia watoto ambao hawana sare za shule na kuwashika mkono ili Hawa watoto waweze kupata elimu Bora” alisema Sagayika.
Kaimu afisa Elimu kata ya Kalangalala Regina Kitau amesema kuwa zoezi la ugawaji madaftari litatoa motisha kwa watoto kufika shule.
Kwa upande wao wazazi wameshukuru uwepo wa zoezi kwani wameweza kupunguza mzigo wa maandalizi ya vifaa vya shule inayotarajiwa kufunguliwa kesho.







