Simba, Singida Black Stars kuna kitu kinaendelea

UONGOZI wa Simba upo katika mazungumzo na Singida Black Stars kwa ajili ya huduma ya beki wa kushoto, Nickson Kibabage ili asaidiane na Antony Mligo ambaye alijiunga na kikosi hicho mwanzo wa msimu akitokea Namungo FC.

Mligo alijiunga na Simba kuziba nafasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ inaelezwa kuwa licha ya kuingia kikosini moja kwa moja hana uzoefu wa kuipambania timu hiyo hivyo wameamua kusaka msaidizi wake ambaye ni Kibabage.

Chanzo cha kuaminika kutoka Singida Black Stars kimeliambia Mwanaspoti kuwa ni kweli Simba wametuma maombi kuhitaji huduma ya Kibabage ambaye amesajiliwa dirisha kubwa akitokea Yanga baada ya mkataba wake kuisha.

“Hadi sasa mazungumzo yamefikia hatua nzuri kama yataenda vizuri basi Kibanage anaingia kwenye vitabu vya kucheza klabu mbili kongwe Simba na Yanga kwani wanamsimbazi wameonyesha nia ya kuhitaji huduma yake,” kimesema chanzo.

SIMB 01

“Uongozi unaendelea kufanya mazungumzo na Simba ili kufanya biashara ya kuwauzia mchezaji huyo ambaye tayari ana uzoefu wa kutosha kutokana na kushiriki mashindano ya kimataifa mara nyingi akipata nafasi ya kucheza.”

Chanzo hicho kilisema lolote linaweza kutokea wao kama timu wapo tayari kufanya biashara wanaisikilizia Simba ambayo ndio inauhitaji wa kumpata beki huyo ambaye wamemtaja kuwa ni hazina kwa taifa kutokana na kujitoa kwake.

“Nafasi anayocheza Kibabage tayari lina mchezaji mwingine ambaye amesajiliwa dilisha hili hivyo kama kutakuwa na biashara hakuna kinachozuia kumtoa mchezaji huyo ambaye Singida ni kama nyumbani alitoka kwenda Yanga na baadaye akarudi hatuna sababu ya kumzuia kwenda timu nyingine yoyote.”

SIMB 02

Mchakato huo wa kusaka beki unafanyika baada ya kocha mkuu wa Simba kuonyesha uhitaji mkubwa wa mchezaji katika nafasi hiyo ya beki wa kushoto (left-back) ili kuongeza nguvu na ushindani kwenye kikosi chake.

Uongozi wa Simba unamvutiwa na Kibabage wakiamini kuwa ndiye mtu sahihi anayeweza kuziba pengo la Tshabalala au kuimarisha eneo hilo kutokana na uzoefu wake katika Ligi Kuu Bara.