NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kubeba Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Azam FC kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Mchezo huo uliisha bila kufungana katika dakika 90 za kawaida na hata baada ya kuongezwa dakika 30 za muda wa nyongeza, ambapo nyavu zilibaki bila kutikiswa na hivyo mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penati.
Yanga ilipata nafasi ya kufunga kupitia penati dakika ya 74 baada ya mchezaji wa Azam FC kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, hata hivyo mpira uliopigwa na Pacome Zouzoua uliokolewa na kipa Aishi Manula.
Katika hatua ya nusu fainali, Yanga SC iliiondoa Singida Black Stars, huku Azam FC ikitinga fainali baada ya kuichapa Simba SC.






