MAADILI NI MSINGI WA TAIFA_ MAGANYA

………..

NA Ester Maile Dodoma 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Fadhili Maganya,amewataka wanafunzi nchini kufuata maadili ya kitanzania na kuepukana na changamoto ya utandawazi iliyopo.

Maganya ameyasema hayo leo Januari 14,2026, alipotembelea Shule ya Sekondari Hombolo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo kwa niaba ya wanafunzi wote nchini.

Hata hivyo amewataka Wanafunzi kuwa na uzalendo ,ushikamano, kupenda Taifa letu Tanzania pia kuongeza bidii katika masomo.