Mshindi wa jumla wa Kampeni ya mwisho wa mwaka ya Magift ya Mixx Pesa iliyoandaliwa na Mixx Bw. Yusuph Constantine Muhoja.
:::::::::::
Mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam, Bw. Yusuph Constantine Muhoja, ameibuka mshindi wa jumla wa shilingi milioni 50 katika Kampeni ya mwisho wa mwaka ya Magift ya Mixx Pesa iliyoandaliwa na Mixx.
Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo imefanyika Dar es Salaam Januari 14, 2026, ikihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Yas na Mixx, wateja pamoja na wadau wa kibiashara wa taasisi hizo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha, alisema kampeni ya Magift ya Mixx Pesa imeleta mabadiliko chanya kwa Watanzania wengi kwa kuwasaidia kulipa ada, kukuza biashara na kuanza maisha mapya.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha.
Alisema zaidi ya familia 40 zimeanza mwaka mpya zikiwa na matumaini mapya, hatua aliyosema inaonesha dhamira ya Mixx ya kuwa mshirika wa kweli wa kifedha kwa Watanzania.
Kupitia kampeni hiyo, jumla ya washindi 44 waliibuliwa kutoka maeneo mbalimbali nchini, wakiwemo washindi 37 wa shilingi milioni moja, washindi watano wa shilingi milioni tano na mshindi mmoja wa shilingi milioni 10.
Mkurugenzi wa Biashara wa Mixx, Bw. James Sumari, alisema kufungwa kwa kampeni hiyo hakumaanishi mwisho wa safari ya Mixx, bali ni muendelezo wa kutoa huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya Watanzania.
Aliongeza kuwa fedha zilizotolewa zitasaidia kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa washindi, huku Mixx ikiendelea kujivunia kuwa sehemu ya safari ya mafanikio ya Watanzania wengi.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hiyo, mshindi wa jumla wa kampeni hiyo, Bw. Yusuph Constantine Muhoja, alisema ameupokea ushindi huo kwa furaha kubwa, akieleza kuwa hakuwahi kuwaza kama kweli watu wanashinda katika kampeni kama hizo, kwani awali aliamini ni taarifa za kupotosha.
Alisema ushindi huo umempa imani mpya na utamsaidia kubadilisha maisha yake pamoja na familia yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha.
Mshindi wa jumla wa Kampeni ya mwisho wa mwaka ya Magift ya Mixx Pesa iliyoandaliwa na Mixx Bw. Yusuph Constantine Muhoja akiwa na mke wake..webp)
.webp)
.webp)



.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
