Misaada huo imetolewa kwa wananchi hao ikiwa ni sehemu ya Zoezi la Medani linalojulikana kama EXERCISE MALIZA linalofanywa na kuruti katika eneo la Msata , kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi na wananchi. Katika tukio kulifanyika zoezi la utoaji huduma za tiba na kugawa vyakula kwa wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myalla, amesema zoezi hilo ni sehemu ya kuonesha Umoja na Mshikamano wa Jeshi kwa wananchi wake, sambamba na jukumu la msingi la Ulinzi wa nchi.
Brigedia Jenerali Myalla amesisitiza kuwa JWTZ litaendelea kushirikiana na jamii inayowazunguka kwa kutoa huduma na misaada ya kibinadamu pale litakapohitajika kufanya hivyo ili kudumisha uhusiano mzuri uliopo.
Aidha, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi, RTS Kihangaiko Meja Edwin Mboya amesema timu ya madaktari na wauguzi wa shule hiyo ilitoa elimu ya tiba na huduma za tiba kwa zaidi ya wananchi 200, ikijumuisha uchunguzi wa afya na ushauri wa kitaalamu.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kihangaiko, Bw. Shabani Mkomo amelishukuru JWTZ kwa kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na wananchi wa Kijiji hicho, akisema misaada hiyo imekuwa na manufaa kwa wananchi hao.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kihangaiko waliopata huduma hizo akiwemo Kibwana Mtiko na Stelah Losai, wameeleza shukrani zao kwa Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali RTS Kihangaiko kwa kuwapatia huduma tiba na vyakula bure, wakisema huduma hizo zimepunguza gharama za tiba kwa wananchi.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea kutoa misaada na huduma mbalimbali kwa jamii kwa lengo la kudumisha na kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi na Wananchi tangu kuasisiwa kwake terehe 01 Septemba, 1964
