Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 16, 2026 ameongoza kikao cha kimkakati na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu wa kisekta, Ofisini kwake, Mlimwa Jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili kuhusu changamoto za biashara kati ya Tanzania na Zambia
Wizara zilizohudhuria kikao hicho ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera Bunge na Uratibu), Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Pia, kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.



