BAADA ya Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kupangwa kundi B ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON), Nahodha wa kikosi hicho, Anastazia Katunzi amesema wanafahamu ugumu na wanakwenda kujipanga.
Mashindano hayo yatakayoanza kupigwa Machi 17 hadi April 3 mwaka huu nchini Morocco na Twiga Stars ikipangwa kundi B pamoja na mabingwa wa mwaka 2022, Afrika Kusini.
Akizungumzia kundi hilo Katunzi amesema wanafahamnu ugumu wa kundi hilo na kama wachezaji wanakwenda kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri msimu huu.
Aliongeza kuwa kupangwa kundi moja na Afrika Kusini kama wachezaji wamechukulia faida kwani sio mara ya kwanza kukutana nao na mara ya mwsiho walipokutana walitoishana kwa sare ya 1-1.
“Afrika kusini mara ya mwisho tulipokutana nao tulitoka sare tunaenda kujipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwa kundi zima na sio timu moja kwa sababu kila timu inajipanga kufanya vizuri,” amesema Katunzi na kuongeza
Katika kundi hilo gumu, Tanzania pia itakabiliana na Afrika Kusini, Ivory Coast pamoja na Burkina Faso huku mechi zote za Kundi B zikipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Al Medina, Rabat.
Hii ni mara ya tatu Twiga Stars inacheza WAFCON mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2010 ilipoishia hatua ya makundi na 2024 pia ilipomaliza mkiani kwenye kundi C na pointi moja.
Kupangwa kundi hilo Twiga Stars kunaiweka kwenye changamoto kubwa, hasa dhidi ya Afrika Kusini ambao ni miongoni mwa timu bora barani Afrika na wenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa.
Hii ni mara ya tatu Tanzania kupangwa kundi moja na Banyana Banyana, Oktoba 31, 2010 zilipokutana kwa mara ya kwanza Stars ilitandikwa mabao 2-1 na 2024 zilitoshana kwa sare ya 1-1.
Hata hivyo ubora wa wachezaji wa Tanzania hasa wale wanaokipiga ligi mbalimbali duniani kunaifanya kundi hilo kuwa gumu kutokana na nafasi za kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake 2027.
Kwa mujibu wa mfumo wa mashindano, timu nne zitakazofuzu hatua ya nusu fainali zitapata tiketi za moja kwa moja kushiriki Kombe la Dunia 2027, huku timu zitakazoishia hatua ya robo fainali zikipewa nafasi ya kuwania tiketi mbili za mchujo.
Morocco, Kenya, Senegal na Algeria
Afrika Kusini Burkina Faso, Ivory Coast na Tanzania
Nigeria, Malawi, Misri na Zambia
Cape Verde, Mali, Cameroon na Ghana