Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Kenani Labani Kihongosi,ametembelea Shina Namba 7 la CCM katika Tawi la Manyoni Mjini, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kimkakati ya kuimarisha uhai wa Chama kuanzia ngazi ya mashina mkoani Singida.
Akiwa katika shina hilo lenye wanachama 150, Ndugu Kihongosi aliwashukuru wanachama na uongozi wa Shina Namba 7 kwa mshikamano, nidhamu na uongozi wao thabiti. Alisisitiza kuwa huo ndiyo utofauti wa CCM na vyama vingine, kwa kuzingatia muundo imara wa Chama, Katiba yake na uongozi madhubuti kuanzia ngazi ya taifa hadi mashinani.
Aidha, aliwasilisha salamu za Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kueleza kuwa hata yeye ameendelea kujifunza misingi ya uongozi bora kutoka kwa viongozi wa mashina, akitaja Shina Namba 7 kama mfano wa uongozi wa karibu na wananchi.
Amewahakikishia wananchi na wanachama wa shina hilo kuwa CCM itaendelea kuleta maendeleo.
Kazi na Utu tunasongambele.
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

