KIHONGOSI AAGIZA WIZARA KULETA AMBULANCE ILONGERO

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amemuagiza Waziri wa Afya Mhe. Mohamedy Mchengerwa kuhakikisha gari la wagonjwa(Ambulance)linafika katika Hospitali ya Wilaya Singida Vijijini haraka iwezekanavyo.

Alitoa rai hiyo leo Jumatatu January 19 baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Singida Vijijini, iliyopo Ilongero, mradi unaogharimu Tsh. bilioni 3.7 katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tano mkoani Singida.


Komredi Kihongosi alimpigia simu Waziri wa Afya Mhe. Mohamedy Mchengerwa na kuigiza wizara hiyo kuhakikisha gari hilo linafika kwa wakati.

Gari hili litarahisisha usafiri wa haraka kwa wagonjwa kutoka tarafa tatu zinazotegemea huduma kutoka hospitali hiyo, na hivyo kuondoa usumbufu mkubwa wa huduma ya afya kwa wakazi wa vijiji vilivyombali.