Chama Cha Mapinduzi kimetaka kumalizwa haraka kwa ujenzi wa Soko la Kimataifala Vitunguu katika Manispaa ya Singida.
Maelekezo hayo yametokewa leo tarehe 19 Januari 2026 na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Kihongosi, alipofanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko hilo.
“Chama Cha Mapinduzi kimetoa maelekezo kwa mkandarasi na Halmashauri kuhakikisha ujenzi wa soko hili unazingatia ubora, kasi na viwango vilivyokubaliwa ili mradi huu wa kimkakati ukamilike kwa wakati na kuwaletea wananchi manufaa yaliyokusudiwa.”Amesema.
Mradi wa ujenzi wa Soko la Kimataifa la Vitunguu unaogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 3.9, hadi sasa umefikia asilimia 20 ya utekelezaji, na unatarajiwa kuboresha biashara ya zao la vitunguu, kukuza uchumi wa wakulima na wafanyabiashara pamoja na kuongeza fursa za ajira mara baada ya kukamilika.
“Miradi ya aina hii ina mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi wa wananchi na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, hivyo lazima isimamiwe kwa umakini na uwajibikaji mkubwa.”alisisitiza Kihongosi.
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za taifa kwa haki na ufanisi.
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)




.jpeg)
