Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkundwe Mwasaga akizungumza na wanahabari katika siku ya pili ya kongamano la Tisa la TEHAMA (TAIC 2026) ambalo limeanza Jan 19 hadi 23 mwaka huu linalojadili mwelekeo wa maendeleo ya kidigitali Dira 2050
………
Vijana nchini wametakiwa kutumia fursa ya kufanya bunifu mbalimbali hasa maeneo yanayohusiana na Akili Unde ili kusaidia uchumi kuwa shindani kikanda na Afrika kwa ujumla.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkundwe Mwasaga katika siku ya pili ya kongamano la Tisa la TEHAMA (TAIC 2026) ambalo limeanza Jan 19 hadi 23 mwaka huu linalojadili mwelekeo wa maendeleo ya kidigitali Dira 2050
Dkt NkunDwe amesema siku ya leo wameifanya ya vijana kwa lengo la kujadili namna vijana wamefanikiwa kupitia bunifu mbalimbali sambamba na matumizi ya akili unde kwani chumi nyingi duniani zinatokana na ubunifu ambao unatolewa na wadau mbalimbali
Akitoa maoni yake katika masuala ya TEHAMA Happy Pascal Mmila Mkurugenzi Mtendaji wa Mmila Teknology Ltd amesema kuwa ni vyema mambo wanayokubaliana yakafanyiwa kazi ili kuongeza faida zaidi kwa taifa.
Kwa upande wao vijana washiriki katika kongamano hilo akiwemo Shabani Kipindula waonyeshaji wa masuala ya Tehama pamoja na Kelvin Erasto Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Mwanzishi wa Rafiki AI wamesema mifungo mingi ambayo wanaifanya wanatumia TEHAMA jambo linalosaidia kufanikisha kampuni zao kukua.
Kongamano hilo linakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ,Mabadiliko ya kidigitali yanayochochea athari za kijamii na uvumbuzi wa kiteknolojia kwa Taifa lenye mafanikio,haki ujumuishi na kujitegemea.

