TADB YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwa mwaka 2026 yameanza rasmi leo tarehe 19 Januari, 2026 katika Viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya fedha, ikiwemo matumizi sahihi ya huduma za kifedha, umuhimu wa kujiunga na mifumo rasmi ya fedha pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiuchumi kwa maendeleo endelevu.

TADB itaendelea kutoa elimu ya ufahamu kuhusu huduma zake, namna inavyofanya kazi katika kuchagiza mageuzi ya kilimo nchini kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara, namna ya kupata mikopo, umuhimu wa urasimishaji wa kilimo-biashara na mfuko wa dhamana ya mikopo kwa wakulima wadogo.