…………
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Haidary Omary Mkazi wa Mtaa wa Pugu Stesheni Kata ya Pugu Stesheni jijini Dar es salaam amekutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwenye mti.
Akizungumza na Torchmedia kwa hisia bibi wa Marehemu Bi.Jevu amesema marehemu alimuaga siku ya Jumatatu akimueleza anaondoka watakutana kwa Mungu kisha akamuachia Shilingi 3000 ampatie mtoto wake na ndipo hakuonekana tena huku mdog6o wa Marehemu ameeleza kuwa wakati mwingine amekuwa hafiki nyumbani kutokana na shughuli zake anazozifanya.
“Siku ya juzi nilimtuma mtoto akamuangalie nyumbani kwake hakumkuta nikajua huwenda labda amekwenda kwenye shughuli zake na ndipo mpaka leo naapata taarifa ya kuwa amefariki kwa kujinyonga”amesema ndugu wa marehemu
Aidha Shuhuda wa Tukio amesema kuwa Marehemu mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa siku ya Jumatatu mida ya mchana.
Kwa upande Mwenyekiti wa Mtaa wa Pugu Stesheni ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Shukuru Mwinjuma maarufu Mgosi amesema matukio kama hayo ya mtu kujinyonga yamekuwa yakijitokeza katika mtaa huo mara kwa mara.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limefika katika eneo hilo na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pugu Stesheni ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Shukuru Mwinjuma maarufu Mgosi akizungumzia tukio hilo

