YANGA imetua nchini Misri tayari kwa dakika 90 ngumu dhidi ya Al Ahly, lakini kabla ya kupaa kutoka Dar es Salaam, kocha Pedro Goncalves ametamka maneno mawili ambayo yatawafurahisha mashabiki wa timu hiyo akisema timu ya kutafuta ushindi wanayo, huku akitaka ushindi au sare ugenini.
Alfajiri ya leo Jumatano Januari 21, 2026, kikosi cha Yanga kikiwa na wachezaji 24 kiliondoka nchini kuifuata Al Ahly huko Misri na tayari kimetua salama. Wachezaji waliosafiri ni makipa Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery na Hussein Masalanga.
Mabeki ni Ibrahim Bacca, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Frank Assinki, Israel Mwenda, Kibwana Shomari, Kouassi Attohoula Yao, Chadrack Boka na Mohamed Hussein.
Viungo ni Mohamed Damaro, Moussa Bala Conte, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Shekhan Ibrahim, Lassine Kouma, Allan Okello na Pacome Zouzoua wakati mastraika ni Prince Dube, Emmanuel Mwanengo na Laurindo Aurélio ‘Depu’.
Akizungumza na Mwanaspoti, Pedro amesema wanajua kwamba wanakwenda kukutana na Al Ahly am-bayo ni timu kubwa kwa rekodi lakini kwa aina ya kikosi alichonacho sasa, Yanga inaweza kupambana na kikosi chochote kwa hesabu za kutafuta ushindi.
Pedro amesema amefurahishwa na aina ya usajili walioufanya kwenye dirisha dogo ambapo wamepata wachezaji ambao wametengeneza timu yenye uwiano sahihi kutokana na ubora wa wachezaji walio-ingia wakichanganyika na wale waliobakizwa.
Yanga imesajili wachezaji watano dirisha dogo wakiwemo kipa Hussein Masalanga, viungo Mohammed Damaro, Allan Okello na washambuliaji Emmanuel Mwanengo pamoja na Laurindo Aurélio ‘Depu’ huku ikiwatoa watatu kwa mkopo Denis Nkane, Celestin Ecua na Mamadou Doumbia ilhali Andy Boyeli ali-yekuwa anacheza kwa mkopo akirudishwa Shekhukhune ya Afrika Kusini.
“Tupo tayari kukutana na Al Ahly ambayo ni timu ngumu na yenye rekodi bora Afrika. Tunawafuata tukijua taarifa zao lakini jambo zuri ni kwamba tuna timu imara, tumefanya usajili uliotufanya kuwa na kikosi kilicho na uwiano mzuri,” amesema Pedro.
“Nina furaha na ubora wa wachezaji wangu, tunakwenda kutumia ubora wa kkosi chetu kutafuta ma-tokeo ya aina mbili tu, kushinda au kutoa sare, haitakuwa mechi rahisi lakini hatuwezi kuwa timu am-bayo itasubiri wapinzani wetu kuamua mchezo.”
Ijumaa Januari 23, 2026, Yanga itakutana na Al Ahly kwenye mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Ma-bingwa Afrika utakaopigwa Uwanja wa Borg El Arab, uliopo jiji la Alexandria nchini humo ambao un-amilikiwa na jeshi.
Timu hizo mbili zimelingana kwa pointi kwenye kundi B la michuano hiyo, zote zikiwa na pointi nne, baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoa sare moja, huku Waarabu hao wakiongoza msimamo kwa tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Pedro amesema ujio wa wachezaji wapya na wale waliokuwepo umeongeza ushindani mkubwa ambapo kila mchezaji ameongeza nguvu ya kupigania nafasi hatua ambayo itawaimarisha kuweza kufanya vizuri.
“Ukiangalia kuanzia mazoezini kuna ari imeongezeka ya kupigania nafasi. Kila mchezaji anajituma zaidi. Hali kama hii itatupa nafasi ya kufanya uamuzi mzuri wa nani aanze au nani acheze mechi ipi. Tuna timu pana ambayo sasa tunaweza kuchagua mifumo bora zaidi lakini kutoa nafasi kwa kila mchezaji kucheza, kama nilivyokwambia tuna mechi nyingi kutoka mashindano tofauti, lazima tuwe na hesabu za ku-wapumzisha wachezaji,” amesema Pedro.
Timu hizo zitarudiana Januari 31, 2026 Yanga ikiwa mwenyeji kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.