Raia wa Msumbiji, Mtanzania kizimbani kwa kilo 20 za skanka

Dar es Salaam.  Raia wa Msumbiji, Seleman Juma Ally (32) ma Mtanzania, Amasha Iddi Mrisho (40), mkazi wa Buza, Dar es Salaam, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke wakituhumiwa kukutwa wakisafirisha dawa za kulevya, aina ya Skanka zenye uzito wa kilo 20.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana jioni,  Alhamisi, Januari 22 2026 , wakasomewa shtaka linalowakabili na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Nicas Kihembe.

Kesi hiyo ya jinai namba 1535/ ya mwaka 2026 imepangwa kusikilizwa na Hakimu Frank Lukosi katika hatua ya uchunguzi wa awali, kukamilisha taratibu za msingi ukiwemo upelelezi kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu Divisheni ya  Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambayo ndio ona mamlaka kisheria kusikiliza kesi kama hizo.

Kwa mujibu wa maelezo ya shtaka hilo, watuhumiwa hao walikamatwa na  maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),  Desemba 8, 2025,   katika mtaa wa Wailes, Temeke, Dar es Salaam.

Mshtakiwa Amasha Mrisho (kushoto ) na raia wa Msumbiji Seleman Ally (kulia) wakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke baada ya kusomewa ya kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Skanka. Picha na James Magai



Walikamatwa na maofisa hao wa DCEA, wakati wakifanya operesheni iliyofanikisha kukamatwa pakiti 20 za dawa za kulevya aina ya  skanka zenye uzito wa jumla wa kilogramu 20.03.

Dawa hizo zilikamatwa zikiwa zimefichwa ndani ya balo la mitumba, ndani  ya basi aina ya Scania la kampuni ya King Masai Tours, lenye namba za usajili wa Msumbiji AAM 297 CA.

Wakili Kihemba  alieleza kuwa  vitendo  cha washtakiwa hao kukutwa wakisafirisha dawa hizo za kulevya ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 16(I) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, inayokataza umiliki, usafirishaji na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Wakili Kihemba aliieleza mahakama kuwa kulingana na uzito wa dawa waliokutwa nazo washtakiwa, shtaka hilo halina dhama

Hata hivyo, wakili Kihemba aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na akaiomba mahakama itoe ahirisho na kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kama sheria inavyoelekeza.

Hakimu Lukosi ailiahirisha kesi hiyo hadi Februari 5, 2026, itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa upelelezi  na akaamuru washtakiwa wapelekwe  mahabusu hadi tarehe hiyo.