Na WANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke, Hamis Slim, amewakata viongozi wa mabaraza, kamati za utekelezaji za kata na matawi za jumuiya hiyo kuvunja makundi yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 , 2029 na kufanyakazi kwa ushirikiano.
Ameyasema hayo Dar es Salaam, leo katika ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo Wilaya ya Temeke katika Kata za Kiburugwa na Kibondemaji inayo lenga kuwashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa ushindi mkubwa wa CCM na kuimarisha uhai wa jumuiya.
Slim, amesema uchaguzi umekwisha hivyo ni wakati muafaka wa kuvunja makundi, kusameheana, kupendana na kuhudumia jumuiya kwa ufanisi na weledi.
“Tunawapongeza Jumuiya ya Wazazi mmeafanya kazi nzuri katika uchaguzi mkuu na kuipatia ushindi wa kishindo CCM na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Sasa ni wakati wa kuleta maendeleo. Tuzike tofauti zetu zilizotokana na uchaguzi. Mwiba ulipoingia ndipo unapotokea,”amesema Slimu.
Pia amewataka kuishi kwa hofu ya Mungu, kuheshimu katiba ya CCM, kanuni na viongozi na wanachama.
“Binadamu anahamika kwa mambo matatu, Jambo la kwanza ni jinsi anavyo jifahamu mwenyewe. Jambo la pili ni namna watu wengine wanavyo mfahamu na jambo la tatu ni nama anavyo fahamika na Mungu. Tusidharauliane kwa sababu mamlaka hata za dunia na viongozi wake zimetoka kwa Mungu,”amesema Slim.
Aidha Slim, ametumia ziara hiyo kutoa pole kwa wanachama wa jumuiya hiyo, CCM na wananchi wote kwa ujumla kwa matukio yaliyojitokeza Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi mkuu na kuwakumbusha umuhimu wa kutunza amani ya taifa.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke, Emmanuel Itatiro, amewataka viongozi wa jumuiya hiyo katika ngazi za mashina, matawi na kata, kutekeleza wajibu wao kwa kufuata Katiba ya CCM na jumuiya hiyo, kanuni na miongozo.
Pia, amewahimiza kuwajibika ipasanyo hususan kuitisha vikao vya kikatiba na kushughulikia changamoto za wananchi, hususa katika sekta za elimu, afya, malezi na mazingira.
Ziara hiyo ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke, itapita katika kata zote za wilaya hiyo.


