Meridianbet Yahakikisha Mazingira Ni Salama Mbezi Juu

MERIDIANBET imeendelea kuthibitisha
kuwa mchango wake hauishii kwenye burudani ya michezo ya kubashiri pekee, bali unagusa
moja kwa moja maisha ya wananchi. Kupitia mkakati wake wa
uwajibikaji kwa
jamii
(CSR), kampuni
hiyo imeshiriki kikamilifu katika zoezi la usafi wa mazingira Kata ya Mbezi
Juu, ikionesha dhamira ya kweli ya kushiriki maendeleo ya kijamii na kiafya ya
wananchi.

Katika kuimarisha mapambano dhidi ya
uchafu na magonjwa yanayotokana na mazingira yasiyo safi, Meridianbet
ilishiriki usafi pamoja na kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi ikiwemo mifagio
imara, mafyekeo, koleo, glovu, mifuko
ya taka pamoja na viatu maalum vya kazi. Msaada huu ulilenga kuendeleza zoezi
la usafi kwa muda mrefu na kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni,
mwakilishi wa Meridianbet Nancy Ingram alieleza kuwa mazingira safi ni
nguzo muhimu ya kuzuia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, homa ya matumbo
na maambukizi mengine yanayohusiana na uchafu. Alisisitiza kuwa Meridianbet inaamini
kuwa jamii yenye afya bora ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna
michezo mbalimbali ya
kasino
mtandaoni
pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri
zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku.
Kujiunga ni rahisi! Tembelea
meridianbet.co.tz au piga
*149*10#.

Diwani wa Kata ya Mbezi Juu
aliipongeza Meridianbet kwa kuonesha ushirikiano wa dhati na serikali za
mitaa katika kulinda mazingira. Alieleza kuwa mchango wa sekta binafsi katika
shughuli za kijamii ni kichocheo muhimu cha uwajibikaji wa pamoja, kwani
huongeza hamasa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda afya zao na
mazingira yanayowazunguka.

Kupitia tukio hili, Meridianbet
imeweka wazi kuwa itaendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii yenye athari
chanya kwa maisha ya wananchi. Kampuni hiyo
imesisitiza kuwa usafi wa mazingira ni wajibu wa kila mdau, na itaendelea
kushirikiana na jamii, viongozi na taasisi mbalimbali kuhakikisha
mazingira yanabaki kuwa salama.