MSHAMBULIAJI wa Ain Diab na Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni, Jaruph Juma ametaja siri ya kuwa na mwendelezo mzuri msimu huu na kuonyesha kiwango bora kwenye Ligi ya Morocco.
Myanzania huyo ambaye alijiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu wa 2024/25, amesema amekuwa akifanya mazoezi binafsi na kujituma kwa misimu miwili na hivyo kuwa bora licha ya kumaliza na mabao 15.
Aliongeza pamoja na chama lake kumaliza nafasi ya tano, haikuwa malengo ya timu inayoshiriki ligi kuu ya soka la ufukweni na ilikuwa ni kutwaa ubingwa.
“Nimekuwa mzoefu sasa ni msimu wangu wa pili, nafikiri malengo ya timu hatukuyatimiza ilikuwa tuchukue ubingwa lakini kutokana na ubora wa ligi, timu zinapambana kweli,” amesema Jaruph.
Msimu wa kwanza mshambuliaji huyo ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa alifunga mabao 10 akicheza mechi nane, msimu uliofuata alifunga mabao 15 kwenye mechi 10.