KIPA wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Peter Manyika Sr amefariki leo alfajiri na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.
Taarifa kutoka kwa kijana wake kipa wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Peter Manyika Jr amethibitisha hilo na kwamba msiba upo nyumbani kwao Mbezi.
“Baba kafariki leo alfajiri, msiba upo nyumbani Mbezi, kwa sasa ni ngumu kusema vitu vingi bado sijatulia,”amesema Manyika Jr.
Kwa upande wa mweka hazina wa taasisi ya wachezaji wa zamani GALACTICOS Idd Moshi, amesema jambo la msingi kwa sasa ni Watanzania kujua kuhusu msiba huo, mengine wasubiri hadi watakapokaa kikao na familia yake.
“Mwenzetu kafariki leo alfajiri, atazikwa lini bado hatuna taarifa hiyo,hadi tutakapokaa na familia yake, mara ya mwisho kikazi alikuwa na Namungo FC,” amesema.
Mbali na kuitumikia Yanga kama kipa na kocha wa makipa, timu zingine alizowahi kuzitumikia ni Yanga, Ihefu Fc, Singida Fountain Gate ,Dodoma Jiji na Namungo.
Endelea kufuatilia Mwanaspoti kwa taarifa zaidi.