• Stanbic inaonesha utaalamu wake kama Mshirika mwenza wa Mpango katika kuunga mkono utoaji wa hivi karibuni wa Sukuk ya Al Barakah ya Benki ya CRDB uliotekelezwa kwa mafanikio.
• Benki inaonesha uwezo mkubwa wa kupanga miundo ya kifedha unaochangia kuimarika kwa mazingira ya masoko ya mitaji yanayokua nchini Tanzania.
• Stanbic inaonesha uzoefu thabiti katika kusimamia miamala na kushirikiana na watoa dhamana wakubwa wa kitaifa.
Dar es Salaam, Tanzania – Ijumaa, tarehe 23 Januari 2026: Benki ya Stanbic imethibitisha tena nafasi yake kama mshirika wa kuaminika katika masoko ya mitaji ya Tanzania kupitia ushiriki wake kama Mshirika mwenza wa uaandaji wa utoaji wa Sukuk ya Al Barakah ya Benki ya CRDB wa hivi karibuni.
Benki ilitoa msaada wa kitaalamu katika upangaji wa muamala mzima, ikitumia uzoefu wake wa muda mrefu na uwezo wake mkubwa wa kikanda kuhakikisha utekelezaji wenye mafanikio.
Sukuk hii ya Al Barakah ya Benki ya CRDB ni awamu ya tatu ambayo Stanbic imehusika kuipangilia kwa niaba ya CRDB, hali inayoonesha ushirikiano wa kudumu uliojengwa juu ya utaalamu wa kina wa kiufundi, upangaji makini na ushirikishwaji mzuri wa wawekezaji.
Kupitia kazi hii, Benki imeisaidia CRDB kuleta katika soko fursa za uwekezaji zinazozingatia misingi ya Shariah, hivyo kupanua wigo wa ushiriki kwa wawekezaji wa rejareja na wa taasisi.
Akizungumza kuhusu utekelezaji huo uliofanikiwa, Sarah Mkiramweni, Makamu wa Rais Mwandamizi, Masoko ya Mitaji ya Deni na Uratibu wa Mikopo kwa Afrika Mashariki, alisema muamala huo unaonesha matokeo chanya ya ushirikiano wa karibu kati ya watoa dhamana, wapangaji na wadhibiti katika mazingira ya kifedha yanayokua.
Aliongeza kuwa timu ya Stanbic itaendelea kujitolea kukuza vyombo vya kifedha vya kimaadili na vinavyoungwa mkono na mali halisi ili kuimarisha masoko ya mitaji ya Tanzania na kupanua chaguo za uwekezaji kwa umma.
Benki ilieleza kuwa uwezo wa upangaji ni muhimu katika soko linalokomaa, hususan wakati Tanzania ikijiandaa kuanzisha mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa fedha za Kiislamu. Kwa uzoefu wa zaidi ya miaka thelathini nchini na uwepo wao barani Afrika, Stanbic inaendelea kuwaunga mkono watoa dhamana wanaotafuta kukusanya mitaji kupitia vyombo vilivyopangwa na kusimamiwa kwa viwango vya juu.
Akizungumzia kuhusu muamala huo, Ester Manase, Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji benki ya Stanbic, alisema mafanikio ya Sukuk ya Benki ya CRDB na Al Barakah yanaakisi kuongezeka kwa imani ya wawekezaji katika bidhaa zilizopangwa kitaalamu na yanaonesha umuhimu wa ushauri imara, maandalizi ya nyaraka na uhamasishaji wa wawekezaji.
Alisisitiza kuwa benki itaendelea kutoa mwongozo unaowasaidia watoa dhamana kubuni vyombo vinavyokidhi mahitaji ya soko na matarajio ya kikanuni.
Stanbic ilibainisha kuwa uwezo wake wa upangaji hauishii kwenye mpango wa Sukuk ya Benki ya CRDB na Al Barakah pekee.
Katika miaka ya hivi karibuni, Benki imehudumu kama Mshirika wa Mpangilio huo wa Dhamana ya Miundombinu ya Samia ya CRDB, kama Muandaaji Mkuu wa Dhamana ya Kijani ya CRDB, pia Mpango Mkuu wa dhamana ya Benki ya NMB iliyoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, na kama Mshirika mkuu wa uandaaji aliyeidhinishwa pamoja na Benki ya Watu wa Zanzibar katika mkopo mkubwa wa pamoja uliolenga kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Stanbic inaendelea kujitolea kuunga mkono ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuimarisha masoko ya mitaji na kuwawezesha watoa dhamana kupata njia bunifu za ufadhili.
Benki inaamini kuwa vyombo vilivyopangwa kwa umakini, vikisaidiwa na wapangaji wenye uwezo, vina mchango muhimu katika kuimarisha uthabiti wa kifedha na kuunga mkono maendeleo ya muda mrefu.

