Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewaagiza TAKUKURU kutengeneza mazingira magumu kwa mtu yeyote anayejihusisha na rushwa ili watu wawe waoga kushiriki vitendo hivyo akihimiza kufanya kazi yao bila woga, bila kuumiza watu ili kuisaidia Tanzania kwani baraka zote za Mkuu wa nchi na Serikali kwa ujumla wanazo.
Waziri Mkuu amesema hayo leo Januari 26, 2026 mjini Morogoro alipomwakilisha Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU ulioanza mjini Morogoro ukitarajiwa kudumu kwa siku nne.
TAKUKURU imetakiwa kuwajenga watoto katika misingi ya kuichukia rushwa na kutambua athari zake tangu wadogo ili kutokomeza vitendo vya rushwa kama ilvyokuwa kwa watoto wa zamani walioweza kuchukia Makaburu ikiwemo kwa nyimbo na hamasa.
Dkt. Mwigulu amehimiza Watanzania kutokuwa na hofu kwenda kwenye ofisi za TAKUKURU hasa kama wana jambo la kuwasaidia badala ya kusubiri kwenda kwenye ofisi hizo kwa wito kwani jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa ni la Watanzania wote.
Related
