Na. Janeth Raphael MichuziTv – Dodoma
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo, amesema kuwa ujio mpya wa stakabadhi za ghala unawakumbusha wakulima changamoto walizopitia kupitia vyama vyao vya ushirika. Aidha, amebainisha kuwa kazi kubwa iliyopo sasa ni kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali na taasisi zake, ikiwemo mfumo huu wa stakabadhi za ghala.
Londo ameyazungumza hayo wakati WRRB Uzinduzi wa Mfumo na kuazimisha Miaka 20 ya Kuimarisha Biashara ya Kilimo Tanzania Kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala 27, 2026, Jijini Dodoma.
Amesema, “Ujio mpya wa stakabadhi ghalani na yenyewe pia inawakumbusha changamoto wakulima hawa kule walikotokea kupitia vyama vyao vya ushirika. Kazi kubwa ambayo nayo sasa hivi ni imani ya wananchi kwa serikali. Imani ya wakulima kwa taasisi za Serikali na mifumo ya Serikali ikiwemo hii ya stakabadhi za ghala.” amesema waziri Londo
AmeelezaAmeeleza kuwa, “Wakulima wanapovuna na kupeleka mazao ghalani, wanategemea malipo mara moja kwa sababu changamoto zao ni kusuluhisha madeni, mikopo, ada za watoto, na huduma za afya. Hata hivyo, wakulima hawa wanaona kama wanakopesha mazao yao kutokana na kucheleweshwa malipo, hali inayotokana na ukosefu wa imani.”
Amesema zaidi kuwa, “Kazi kubwa ambayo mnafanya ni jema katika kumkomboa Mtanzania hasa mkulima mdogo kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala. Umeongeza ushindani, umeongeza uwazi, na umefanikiwa kuhakikisha kwamba tunalinda ubora wa mazao yetu.”
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na uwajibikaji katika utekelezaji wa mfumo huo kwa kusema, “Hatuwezi kufikia malengo kama hatuta lazimisha masoko yetu ambayo kimsingi ndiyo yanatumika kama ulinzi kwa wakulima wetu. Ni lazima kila mmoja ahakikishe tunabadilisha mind set ya Watanzania kuhusu suala zima la stakabadhi za ghala.”
Mhe. Londo pia amewataka watumishi wa stakabadhi za ghala kusimamia ushirikiano wa karibu na sekta binafsi, akibainisha kuwa, “Hatuwezi kufanikisha bila ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa shughuli za kila siku. Ni lazima tutaidentify stakeholders na kuwaratibu ili kufanikisha majukumu yetu.”
Ameongeza kuwa, “Kama tukisubiri watumishi wa kutosha, hatutaweza kusimamia vizuri katika ngazi za halmashauri na usimamizi utakuwa hafifu.”
Mhe. Denis Londo amehitimisha kwa kusema, “Na sisi tuna bahati kuwa tunatumikia nchi yetu na kuitendea haki Serikali yetu. Tutende haki Rais wetu. Kila mmoja akitimiza wajibu wake, tutafanikiwa.”
Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu, amesema kuwa mfumo wa stakabadhi za ghala umeleta mafanikio makubwa katika miaka ishirini, ikiwemo kuboresha bei, kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa.
Aidha, amebainisha kuwa bidhaa kumi na nane sasa zinatekelezwa kupitia mfumo huu na mpango wa kuongeza bidhaa zisizo za kilimo kama mifugo, uvuvi, na madini unatekelezwa.
Aidha, amebainisha kuwa maadhimisho ya miaka ishirini yatafanyika mwezi wa 4,2026 , ambapo watashirikisha wadau waliokuwa wakifanya kazi pamoja na kuwapa elimu wanafunzi na wakulima kuhusu mfumo huo.