TET YASHIRIKI KUPANDA MITI KUMBUKIZI YA KUZALIWA KWA RAIS DKT. SAMIA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba ameongoza Menejimenti ya Taasisi ya Elimu Tanzania kupanda miti ili kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira katika kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 27/01/2026.

Kwa niaba ya Menejimenti na watumishi wa TET, Dkt. Komba amemtakia Mhe. Rais, heri katika siku yake ya kuzaliwa, pia kumtakia maisha marefu.

Akiongoza zoezi la upandaji miti Dkt. Komba amesema, TET inaendelea kuenzi kwa vitendo siku hii kwa kufanya zoezi hilo la kupanda miti kama sehemu ya maudhui katika somo la Jiografia na Mazingira kwenye Mtaala ulioboreshwa Elimu ya Msingi.