-Azindua wa mfumo wa kidigitali wa ‘Ongea na Waziri’,
-Asisitiza umuhimu wa uwajibikaji ,utu kwa wahudumu , awataka kuzingatia maadili
Na. Vero Ignatus Arusha
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ametoa maagizo kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuanza rasmi ujenzi wa jengo la gorofa katika Kituo cha Afya Kaloleni, hatua inayolenga kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaofika kupata huduma katika kituo hicho.8
Akizungumza hayo Leo Jumatatu Januari 26, 2026 jiji Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho, Waziri Mchengerwa amesema ongezeko la wagonjwa limefanya miundombinu iliyopo kushindwa kukidhi mahitaji, hivyo ujenzi wa gorofa ni hatua muhimu ya kuboresha huduma na kuongeza ufanisi.
Akizindua wa mfumo wa kidigitali wa ‘Ongea na Waziri’, Mhe. Mchengerwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Dkt. Seif Shekalaghe kuanza mara moja mchakato wa kukipandisha hadhi kituo cha afya Kaloleni ili kuwa Hospitali ya Wilaya, akionesha kuridhishwa na utoaji wa huduma na uwekezaji mkubwa wa Vifaatiba katika Kituo hicho.
Aidha, ametoa maagizo mahsusi kuhakikisha huduma zote za dawa na zinapatikana ndani ya kituo hicho, akisisitiza kuwa hakuna mgonjwa anayepaswa kupelekwa kununua dawa nje ya kituo, kinyume na maelekezo ya serikali na kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati licha ya changamoto zilizopo.
Asiwepo Daktari wa kumuandikia mgonjwa kwenda kununua dawa nje ya hospitali, hatuna changamoto ya dawa MSD inajitosheleza kuleta dawa aina zote, pia nakemea tabia ya baadhi ya na Daktari kuwa na maduka yao ya dawa ambayo mnawaagiza wagonjwa wakanunue dawa, nakuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Dkt. Seif Shekalaghe zoezi hilo la ufustiliaji lkuanza mara moja. Alisema.
Waziri Mchengerwa amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji na utu kwa wahudumu wa afya, akiwataka kuzingatia maadili ya kazi na kutumia lugha nzuri na yenye staha kwa wagonjwa, kwani huduma bora huanza na mawasiliano mazuri.
Ameongeza kuwa, endapo ujenzi wa kituo hicho cha afya utakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa, Serikali itaipandisha hadhi Kituo cha Afya Kaloleni kuwa Hospitali ya Wilaya, kutokana na sifa zake za kuwa na vifaa vya kisasa na uwezo wa kutoa huduma zote muhimu za afya.
“Wizara yake itaendelea kushirikiana pia na Mkoa kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora kwa wananchi, wageni na watalii na kuendana na upekee wa Mkoa wa Arusha katika sekta ya Utalii na ujio wa michuano ya mpira wa miguu ya AFCON 2027′ Alisema
Waziri Mchengerwa amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji na utu kwa wahudumu wa afya, akiwataka kuzingatia maadili ya kazi na kutumia lugha nzuri na yenye staha kwa wagonjwa, kwani huduma bora huanza na mawasiliano mazuri.
Waziri wa Afya nchini Tanzania Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itajenga Jengo la ghorofa kumi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, katika jitihada zake za kuimarisha sekta ya afya Mkoani Arusha na kuufanya Mkoa huo kuwa na uwezo zaidi katika kuhudumia wananchi.
Awali katika maelezo yake, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Amos Gabriel Makalla amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya afya, akiwapongeza na kuahidi kushirikiana na watoa huduma za afya Mkoani hapa katika kutimiza dhamira njema ya Rais Samia katika kuhudumia wananchi wa Mkoa wa Arusha.



