HABARI PICHA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI – IDARA YA SUKI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndg. Rabia Abdalla Hamid,leo tarehe 28 Januari, 2026, amekutana na Katibu wa Pili – Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini,Bw. Jack Fenwick.

Bw. Jack amefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano.