Mbunge wa Momba Aishinikiza Serikali Kupunguza Gharama za Intaneti – Video

Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe kwa mara nyingine ameibua suala la gharama kubwa za mabando na intaneti, zinazosababisha ugumu kwa wafanyabiashara wa kidigitali na kuiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama hizo.

Condester ameelekeza swali lake kwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo naibu waziri wa wizara hiyo, Switbert Mkama amejibu swali hilo kabla ya Spika Mussa Azan Zungu kupigilia msumari hoja hiyo.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.