Tume yakutana na wataalam wa patholojia, vilipuzi

TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 28, 2026, imekutana na mtaalam wa uchunguzi wa patholojia Dkt Ahmed Mattaka pamoja na mtaalam wa vilipuzi Inspekta Raphael Maira.

Mkutano huo wa Tume na wataalam hao umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo kulingana na utaalam wao.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ikiwa na lengo la kupata kiini cha chanzo cha matukio hayo na kuyawasilisha kwa ajili ya hatua zaidi.