::::::::
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini mwalimu mhakiki wa maandishi ya Breili na michoro ya mguso kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania Hadija Salum wakati akitoa maelezo kuhusu matumizi ya michoro ya mguso katika ufundishaji wa watoto wa awali, wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili, mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Baraza la mitihani (NECTA) leo Januari 29, 2026.