BANK of Africa Tanzania (BoA) imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Huduma ya Kifedha yaliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango yaliyofanyika katika viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga.
Yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi,” malengo makuu ya maadhimisho hayo yalikuwa ni kuongeza uelewa, kuboresha ufahamu na hatimaye kuhamasisha mabadiliko ya tabia za wananchi katika usimamizi wa fedha na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.
Aidha, tukio hilo lililenga kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma rasmi za kifedha kama sehemu ya jitihada za kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii, ili kufikia maendeleo ya kiuchumi jumuishi na endelevu.


Washiriki wa Wiki ya huduma ya kifedha kitaifa wakiwa kwenye wakiwa kwenye Banda la Bank of Africa Tanzania (BoA) katika viwanja vya Usagara,jijini Tanga juzi.