Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amekutana na kuzungumza na Mrajis wa Jumuiya kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ahmed Khalid Abdulla lengo ikiwa ni kuimarisha utaratibu wa pamoja wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.
Aidha Mrajis huyo amekutana na kuzungumza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Vickness Mayao wakijikita katika kuweka Mashirikiano kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu na utekelezaji wa majukumu yao kwa uwazi, ufanisi na kwa mujibu wa sheria zote mbili.
Kikao hicho cha Robo Mwaka kimefanyika tarehe 29 Januari, 2025 katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma, ambapo pia wamejadili masuala muhimu yanayohusu usajili na usimamizi wa NGOs nchini.






